December 3, 2008 December 3, 2008 December 3, 2008 بعثه مقام معظم رهبری در گپ بعثه مقام معظم رهبری در سروش بعثه مقام معظم رهبری در بله
December 3, 2008 December 3, 2008 December 3, 2008 December 3, 2008 December 3, 2008

December 3, 2008

KWA JINA LA MWENYE ENZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU   Ardhi ya wahyi kwa mara nyengine imelikusanya tena kundi la wageni wake kama ifanyavyo katika kila mwaka. Nafsi zenye kiu ya mapenzi kutoka pande zote za dunia zimekusanyika

KWA JINA LA MWENYE ENZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
 
Ardhi ya wahyi kwa mara nyengine imelikusanya tena kundi la wageni wake kama ifanyavyo katika kila mwaka. Nafsi zenye kiu ya mapenzi kutoka pande zote za dunia zimekusanyika kwenye kitovu cha Uislamu na Qurani, huku zikiwa zimeshughulika katika kutenda ibada ya Haji, na ukitafakari katika suala hili utaiona ile siri ya kubaki kwa Qurani na Uislamu kwnye nafsi za wanaadamu, na hii ni darsa kubwa kwa Waislamu.
Na lengo kubwa la darsa hii ni kuwapa wanaadamu ile sifa yao ya asili ya utukufu ,kwani mwanaadamu ni kiumbe aliyetukuzwa na Mola wake.na njia ya kuwafikisha wanaadamu katika sifa hiyo, kwanza ni kumpa mwanaadamu malezi sahihi ili iweze kupatikana jamii ilio sahihi isio na matatizo, na kwa kufanya hivyo ndipo atapopatikana yule mwanaadamu ambaye kimatendo na kimoyo anaendana na amri za Mola wake, ili aisafishe nafsi yake kutokana na ushirikina, tabia zilizo ovyo pamoja na matamanio ya nafsi yaliopambwa na Shetani, na kukipatikana mwanaadamu mwenye sifa hizi, hapo ndippo itapopatikana jamii ilio na uadilifu, uhuru, imani pamoja na maendeleo tofauti ya kijamii.
Ndani ya ibada ya Haji mna misingi mikuu ya kumlea mwanaadamu mmoja mmoja na vilevile jamii nzima, ukianzia kwenye kuvaa nguo ya ihramu hadi kufika katika kutufu (kuizunguka Kaaba) na mwishowe kuzivua nguo za hija, yote hayo yanamkaribisha mwanaadamu mbele ya Mola wake, kwa kule kujitenga na matamanio ya nafsi yake. Na ukiangalia kule kukimbia baina ya Safa na Marua hadi kufikia Arafati kwenye kundi kubwa la wacha Mungu walio na rangi tofauti na kabila tofauti na kule kubaki usiku Mina na vile vile kuhudhuria hapo Mina na kumpopoa Shetani na bila ya kusahau kule kutoa kichinjwa na kuwalisha maskini na wenye kuhitaji pamoja na wapita njia, yote hayo basi  ni mazowezi, ukumbusho na mafuzo kwa muumini. Ukiangalia mafunzo haya utakutia kwa upande mmoja kuna ikhlasi na usafi wa moyo na  kwa upande mwengine ni kuiipa mgongo dunia na kujisogeza kwa Alla (s.w) na kwa upande mwengine ni kuunga mkono umma wa kiislamu, na vilevile kusimama kidete katika kuupinga upotofu huku akimimina uzito kwenye mezani ya akhera huku akiipa mgongo dunia. Yote haya basi yamo kwenye ibada ya Hija.
Mwenye Enzi Mungu katika Quran anasema: (Mwenye Enzi Mungu ameijaalia Kaba na ibada ya Haji kua ni nguvu na rasili mali kwa ajili ya watu na ni manufaa kwao …..) 
Waislamu leo wanatakiwa kuiipa umuhimu zaidi ibada hii kwa kutokana na umuhimu wake ilio nao kwani wingu lililoufinika uislamu katika ulimwengu wa leo ni lenye kupambazuka, na macho ya waislamu yamo katika kuisubiri faraji na waislamu wanatarajia kuyafikia malengo yaliowekwa na uislamu. Ikiwa uislamu kwenye karne mbili zilizopita umekumbwa na wimbi la mvurugiko na kushindwa mbele ya utamaduni wa kimagharibi na mila za kipagani, huku ukiwa uislamu huo umesimamiwa na maadui kuliani kwake na kushotoni kwake, lakini leo tukiwemo kwenye karne ya kumu na tano Hijiria maadui wa uislamu kitamaduni na kisiasa wamekabiliwa mvurugiko.
Na uislamu kwa kutokana na msimamo wa waislamu umeweze kuirudisha picha yake iliokua imegubikwa na vumbi la matatizo tofauti, hili limepatikana kwa kutokana na kule kuyatandaza duniani mafunzo ya Tauhidi na uadilifu wa uislamu, leo basi uislamu uko katika zama mpya za kujitangaza kwa mara nyengine tena.
Maadui jana walikua na ndoto ya kuusomea faatiha uislamu na kulikunja jamnvi la uislamu huo, lakini leo macho yao yamefumba na nuru itokayo kwenye ua jengile jipya lililoanza kuchanua hivi karibuni na wao wenyewe wanalikubali hilo kwa nyoyo zao pamoja na ndimi zao, na leo nasema kua huu ni mwanzo wa kazi, na litaendelea jambo hilo hadi kuufikia mchana wa uislamu na kudhihirika ile ahadi ya Alla (s.w) aliowaahidi waja wake kua atawafanya wao kua ndio watawala wa ardhi hii kama vile alivyowafanya waumini waliopita……
Na mfano mzuri wa kubigwa hapa Irani pale serikali ya kiislamu ilivyokamata hatamu na kubadilika kua ni moja kati ya nguvu kuu za uislamu diniani na kua ni kituo kikuu katika kuusambaza utamaduni wa kiislamu duniani, na jambo hili ukiliangalia utaliona kua ni moja kati miujiza, kwani serikali hii inahujumiwa katika pande zote, kiuchumi kitamaduni na kisiasa lakini hadi leo utaiona kua bado inazidi kusonga mbele kwa nguvu za Mwenye Enzi Mungu, na moja kati ya miongoni mwa matunda yakiopatikana ni kupatikana misimamo katika nchi tofauti duniani, kama vile Palestina Afrika pamoja na nchi nyengine za mashariki ya kati, bila ya kuusahau msimamo na ushindi wa kitarehe wa Hizbul-Lla dhidi ya Mazayuni wa Kiyahudi,
na kwa upande mwengine ni kupinduka utawala wa kidikteta wa Sadam au ushindi wa Afghanistani dhidi ya Komonisti pamoja na kushindwa Mmarekani katika ujanja wake wa kutaka kuitawala Mashariki ya kati, ambalo jambo hili kwa Mayahudi ni donda lisilo na dawa.
Kwa hiyo basi kushindwa kwa Mmarekani pamoja na Myahudi na kule kuendelea serikali ya kiislamu katika nyanja tofauti pamoja na vijana kuukumbatia uislamu na wataalamu mbali mbali kushikamana na uislamu, hizi ni dalili wazi zenye kuonyesha  maendeleo ya uislamu duniani na hili ndilo lililowafanya vijana na wazee wa kimagharibi kuukubali uislamu  na hii ni dalili ya ushindi.
Enye ndugu zangu wakike na wakiume, ushindi huu haukupatikana isipokua kwa 
 Kupitia Jihadi (jitihada) na Ikhlasi, kwani Mwenye Enzi Mungu anatuambia : (zitekelezeni ahadi zangu nami nikutekelezeni yale niliyokuahidini….) na kwenye aya nyengine anasema: (mkimnusuru Mola wenu basi naye atakunusuruni na takuthibitisheni kwenye dini yake).
Kwa hiyo huu ni mwanzo wa njia kwani waislamu bado wamejawa na vumbi vichwani mwao, na vumbi hili haliwezi kuondoka bila ya kua na imani pamoja na ikhlasi, na bila ya kua na matumaini na kujitahidi huku tukiwa macho katika kusubiri si  rahisi kuweza kuyafikia malengo yetu. Na tukikaa kufuga mikono na kuyaangalia mambo yaendavyo bila ya kuhisi kua kuna tofauti yeyote huku tukikata tamaa na kuto kuzingatia ahadi aliyotupa Mola wetu (s.w) basi hatuwezi kufika popote.
Basi tuwe makini kwani adui aliyejeruhiwa na uislamu tayari amezikusanya nguvu zake zote na yupo uwanjani kwa ajili ya mapambano, kwa hiyo basi tunatakiwa kuwa macho na kuchukua tahadhari pamoja na kutafuta nafasi ilio wazi ili kuijaza kwa  mashambulio huku tukiwa mashujaa, hapo ndipo tutapompigisha magoti adui yetu.
Mapigo makali ya adui mara nyingi hua ni dalili ya kushindwa na kutokua na mpangilio katika mashambulizi, tukianzia Palestina hasa hasa upande wa Ghaza tutakutia dhulma zinazopita huko ni kubwa mno zenye kupigiwa mfano kitarehe, kushindwa kwa Mayahudi kunatokana na msimamo wa Wapalestina, na hilo basi ndilo lililowasababisha maadui kushindwa, na maadui wakuu leo ni Mmarekani na Myahudi, na Wapalestina leo wameifahamu na kuitumia vyema aya isemayo: (tutakujaribuni kwa kukupeni matatizo, njaa, upungufu wa mali, vifo pamoja na upungufu wa mazao, na bishara njema ni kwa wenye kusubiri…)
Na mshindi kwenye mieleka hii bila shaka atakua ni haki, kwani siku zote haki iko juu na batili itabaki kua chini, na Wapalestina katika vita hivi ndio watakaoshinda kwani Mwenye Enzi Mungu mtukufu na mwenye nguvu.
Leo uongo wa Mmarekani anaodai kua anataka kuleta Demokrasia duniani umedhihirika, na si yeye tu aliyefedheheka bali hata nchi nyengune za kimagharibi zinazokubaliana nae nazo pia zimefedheheka, kwani siku zote wanadai kua wanatetea haki za wanaadamu duniani, na hakuna njia ya kuzifinika aibu zao, basi siku hadi siku watazidi kudidimia.
 
 
Sayyed Ali Al-Hossein Al-Khamenei
4 Zil-Hajja, 1429
December 3, 2008


| شناسه مطلب: 11411







نظرات کاربران