3 Dhil-hija lharam 1430 3 Dhil-hija lharam 1430 3 Dhil-hija lharam 1430 بعثه مقام معظم رهبری در گپ بعثه مقام معظم رهبری در سروش بعثه مقام معظم رهبری در بله
3 Dhil-hija lharam 1430 3 Dhil-hija lharam 1430 3 Dhil-hija lharam 1430 3 Dhil-hija lharam 1430 3 Dhil-hija lharam 1430

3 Dhil-hija lharam 1430

    Bismillahi Al-rahmani Al-rahimi   Wala hawla wala kuwata illa billahi al-aliyyu l-adhim   Msimu wa Hija ni kipindi kizuri chenye utukufu na ni kipindi ambacho kinainawirisha dini ya kiislamu kati

 
 
Bismillahi Al-rahmani Al-rahimi
 
Wala hawla wala kuwata illa billahi al-aliyyu l-adhim
 
Msimu wa Hija ni kipindi kizuri chenye utukufu na ni kipindi ambacho kinainawirisha dini ya kiislamu katika ulimwengu mzima. Hapana shaka ibada ya hija inamfanya mwenye kuhiji aepukane na maasi au madhambi aliyoyafanya kwa kughafilika  au kwa makusudi na Mwenyeezi Mungu humjaalia nuru mwenye kuhiji kurudi akiwa hana madhambi au makosa yoyote, mwenye kuhiji huachana na nguo ya kifakhari , na wanaohiji wote hudhihiri wakiwa na nguo moja tu (nyeupe)  nguo hiyo ni alama inayoonesha umoja wa waislamu. Na hii inaonyesha kwamba waislamu wote wanafuata yale ambayo Mola wao amewaamrisha. Na waislamu wote kuwa kitu kimoja katika shida na raha katika ulimwengu mzima.
          Allah (sw) kuhusiana na msemo wa hija anasema:-
 
Failahukum ilahu wahiduu falahu aslimuw wabashiri lmukhbitiyn.yaani:-
 
Mola wenu ni Mola mmoja tu mkubalini na mumtii, na wabashirieni wale watu ambao wenye hudhui na hushui mbele ya Mola wao. Na kwa upande mwengine:-
"Na Masjidi l-haram ni (msikiti mtukufu) ambao Mwenyeezi Mungu amewajaalia watu wote ulimwenguni, wale ambao wako ndani ya Makka na wale ambao wako mbali na Makka, vile vile  mbali ya kuwa Mwenyeezi Mungu amelichaguwa Kaaba kuwa ni alama ya tawhiyd (kuwa na imani ya mola mmoja) vile vile ni alama inayoonesha umoja udugu na usawa kwa waislamu wote duniani.
Waislamu wote ambao wamekusanyika katika sehemu hii tukufu wamekuja kutoka sehemu mbali mbali za dunia wakiwa na shauku na upendo wao wenyewe kutaka kulitufu kaaba na kulizuru kaburi la Mtume Muhammad  (s.a.w) basi waislamu wote ni lazima waitumie fursa hiyo ili kuthibitisha udugu umoja na usawa uliopo baina ya waislamu wote duniani. Na hii itawapelekea waislamu wote kuneemeka na kutafuta njia ya kusaidiana katika umati wote wa kiislamu duniani.
Katika kipindi hiki maadui wa kiislamu walioko katika pande zote za dunia wamejigawa katika sehemu zote wanazoishi waislamu wakifanya udhalimu wao kidhahiri,(kiuwazi), angalieni Palestina imekabiliwa na mahabithi wa kisehyunist na bado wanaendelea kuishi katika maisha ya tabu. Angalieni msikiti wa (Masjidi) Aqsa uko katika hatari, na angalieni watu wa ghaza wanavyodhulumiwa na mauaji yanavyoendelea kiasi cha kwamba mauaji hayo hayajapata kutokea katika kipindi cha nyuma na watu wa ghaza wanaishi katika maisha mabaya na ya tabu kabisa. Angalieni Afghanistan kila siku madhalim wanazidi kuwaletea misiba. Iraq hawana utulivu na hawana raha ya maisha. Na katika kipindi hiki cha sasa hivi ndugu zetu wa Yemen wanauliwa kiholela hii imewafanya waislamu wote duniani kuwa na huzuni.
Waislamu wote duniani inawapasa kufikiri ili kuelewa fitna vita, maripuko na mauaji yanayozidi kuendelea, katika miaka hii ya sasa hivi  katika nchi za Iraq, Afghanistani, na Pakistani yanasababishwa na nini? Kwa nini kabla ya kuingia  watu ambao wanadai kuwa ni mahakimu na kabla ya kuja jeshi la nchi za kimagharibi (nchi za Europe) jeshi ambalo limetayarishwa na watu wa Marekani watu wanchi hizo hawakuwa na misiba yoyote?
Kwa upande mwengine madhalimu wanadai kwamba kujitetea na kudai haki zao watu wa Palestina, Lebanon, madhalimu hao wanadai kwamba watu hao ndio terurist? Na kwa upande mwengine terurist wa kweli wamejenga  makabila baina ya watu wanchi hizo na kuwatawala, sehemu za midlle east na Afrika ya kusini katika kipindi kirefu na zaidi ya karne moja nchi hizo ambazo zimetajwa hapo juu ziko mikononi mwa dola za kimagharibi:- kwa mfano London, Fransa n,k … vile vile nchi hizo ziko mikononi mwa Wamarekani wakidhulumiwa na kudharauliwa. Maadini asili ya watu wanchi hizo yamechukuliwa vile vile uhuru wao pia umechukuliwa.
Mila na wananchi wanchi hizo wanahujumiwa na kutekwa na watawala wa Kimarekani, lakini baada ya kuamka na kushtuka kwa waislamu katika kupigania haki zao, kugutuka kwa waislamu kumewapelekea madhalimu waelewe kuwa haiwezekani tena kuendelea na dhulma zao juu ya waislamu, tendo la kupigana jihadi kwa ajili ya kupigania haki za wanaadamu na kwa ajili ya Mwenyeezi Mungu vile vile ni dalili inayoonesha kwamba waislamu wako thabiti juu ya kuihifadhi dini yao,jambo la kushangaza ni kwamba madhalimu hao baada ya kugunduwa kuwa haiwezekani tena kuwadhulumu waislamu kwa njia ambazo walikuwa wakizitumia hapo mwanzo sasa hivi wamevumbuwa njia nyengine ili kufikia katika malengo yao.
 Katika kipindi hiki madhalimu ambao wana tabia za kishetani wanafanya kila jitihada ili kuwafanya waislamu wawasikilize na kwafuata na kuwapigia magoti  wao (kuwanyenyekea).
Madhalimu hao wanatumia nguvu za kijeshi, kueneza habari za uongo ili kufikia katika malengo yao.
Makundi hayo ya kidhalim yanaendelea kufanya mauaji ya kikatili bila ya huruma na wanaeneza tabia mbaya za kifisadi, na kuzidisha kueneza madawa ya kulevya na kuharibu tabia za vijana katika jamii. Madhalimu hao wanahujumu sheria za kisiasa katika sehemu ambazo kuna watu thabiti wanaojihami na kupigania haki zao ili kuleta hitilafu na kujenga uadui baina ya watu na waislamu kwa ujumla.
Pindi itakapokuwa waislamu wote wataondowa hitilafu zao na wakajenga upendo, huruma na fikra nzuri baina yao badala ya kuweka fikra mbaya baina yao wenyewe fikra ambazo zinawapelekea madhalimu na maadui wa kiislamu kufikia katika malengo yao, basi kama waislamu watakuwa kitu kimoja itapelekea kuyafanya malengo mabaya ya madhalim (ambayo ni kuwaweka waislamu mikononi mwao)yasifanikiwe.yaani:-
(kiongozi wa kiislamu katika dunia nzima anawashauri (anawataka) waislamu wote wawe kitu kimoja ili kuulinda uislamu).
Hija ni moja katika fursa bora inayopelekea kuleta madhumuni (hadafu) haya yafuatayo:-
Pindi itakapokuwa waislamu ni kitu kimoja, na wakaegemea au kuzingatia yale ambayo wanashirikiana kwa kufuata Qur-ani na sunna itawafanya wawe na nguvu na kusimama kukabiliana na madhalimu wenye fikra za kishetani, na kwa kufanya hivyo basi kutawapelekea kuwaghilibu na kuondoa matakwa na imani za madhalimu.
Jamuhuri ya kiislamu ya Irani kwa kufuata darasa za Imam Khumeini (r.a) imeonyesha mifano iliyo wazi iliyowapelekea kufanikiwa katika mapinduzi ya kuikombowa nchi yao. Madhalimu wameshindwa katika nchi ya Irani, karibu ya miaka thalathini madhalimu wametumia teknik (program) na kufanya uadui katika mapinduzi na kuhimili vita visivyopunguwa miaka minane, ili kuondowa vitengo vya kiuchumi na kukuleta propaganda za vita ili kuwaathiri watu kiakili na kinyoyo, madhalimu hao wamejiweka safu moja ili kuzuia ukuwaji wa kielimu na kuzuia elimu ya juu,Kwa mfano:-
Elimu ya Nuclear, vile vile madhalim wanajitahidi kuingilia na kuonyesha kwa uwazi uadui wao na kwa kuthibitisha kauli hiyo tumeshuhudia uchaguzi wa miaka ya mwisho (uchaguzi wa Iran) watu wote katika sehemu zote wameshuhudia kushindwa kwa madhalimu hao. Kama vile Allah (s.w) anavyosema:-
Kwa hakika kaidi (matakwa, malengo) ya shetani tangu hapo mwanzo yalikuwa dhaifu. Na katika kila sehemu nyengine ya dunia  waislamu wamesimama thabiti wakiwa na malengo na imani  ili kukabiliana na watu madhalimu kwa ajili ya kupigania haki zao.
Hakuna shaka kwamba siku zote mafanikio na (kufaulu) ni kwa ajili ya wenye imani na kushindwa ni kwa madhalim.
Mafanikio ya jihadi ya siku thalathini na tatu yaliyoshuhudiwa miaka mitatu ya mwisho katika mji wa ghaza yanathibitisha kwa uwazi kabisa uhakika huo.  Nasaha ambazo amezitowa Kiongozi wa Irani kwa mahujaji wote duniani waliopata saada hiyo tukufu (ya kuhiji) na zaidi kwa maulamaa na wahutubiaji wa kidini katika nchi zote za kiislamu ambao wamehudhuria katika katika ibada hii tukufu , na kwa wale maulamaa ambao wanahutubia katika misikiti ya sala ya ijumaa katika msikiti wa Makka na Madina inawawajibikia kufahamu kwa vizuri yale mas-la ambayo inawawajibikia katika kipindi hiki (yaani kuwafahamisha watu ni nani maadui wao)  Maulamaa na wahutubiaji ni lazima wawe pamoja ili kuondoa propaganda ambazo zinapangwa na maadui wa kiislamu na vile vile inawapasa kuwaeleza watu na kuwataka wawe pamoja na kuwa kitu kimoja na kila dhana mbaya ambayo inayowapelekea waislamu kuhitilafiana ni lazima wawafahimshe kujiepusha na dhana hizo , na kuwataka wawe na hadafu asili ambayo ni kuwapiga vita madhalim na maadui wa kiislamu kwa sababu chanzo cha fitna zote hizi ni sehyunist na Amerika.
Na waislamu wote inawapasa kutokubali na kupinga matakwa ya watu madhalimu ambao ni washirikina  nakutokubali huko ni ni lazima kuwe katika maneno na vitendo.
Imam Khumeini anasema :-
Anamuomba Mwenyeezi Mungu yeye mwenyewe na waislamu wote kwa ujumla popote walipo awaongoze katika njia njema na kuwapa tawfiq kuwasaidiana kuwazidishia rehma katika maisha yao yote.
 
 
Wasalamu alaykum warahmatu llahi taala wabarakatuh.
 
                                                                          Sayyid Ali Husseyni Khamenei
                                                                             3 Dhil-hija lharam 1430


| شناسه مطلب: 11421







نظرات کاربران