8 11 2010 (A.D) 8 11 2010 (A.D) 8 11 2010 (A.D) بعثه مقام معظم رهبری در گپ بعثه مقام معظم رهبری در سروش بعثه مقام معظم رهبری در بله
8 11 2010 (A.D) 8 11 2010 (A.D) 8 11 2010 (A.D) 8 11 2010 (A.D) 8 11 2010 (A.D)

8 11 2010 (A.D)

بسم اللَّه الرحمن الرحیم والحمدلله رب العالمین و صلی الله علی سیدنا محمد المصطفی و آله الطیبین و صحبه المنتجبین Baada ya shukranı na kumtakıa rehma na amani Mtukufu Mtume (s a w w) alisema; Kaaba ni ishara ya umoja na mshikamano na ni al

بسم اللَّه الرحمن الرحيم
والحمدلله رب العالمين و صلي الله علي سيدنا محمد المصطفي و آله الطيبين و صحبه المنتجبين
Baada ya shukranı na kumtakıa rehma na amani Mtukufu Mtume (s a w w) alisema;
Kaaba ni ishara ya umoja na mshikamano na ni alama ya tawhiidi na uongofu wa kiroho pia Kaaba ni mwenyeji  wa nyoyo zilizo na upendo na matumaini, nyoyo ambazo zimekusanyika kutoka pande zote duniani zikiitika wito wa Mola wao mtukufu kwa (لبيك ) ambayo ni  maneno ya waliopo katika ardhi ya chimbuko la Uislamu. 
Uislamu hivi sasa unaelezea uwezo wake katika nyanja tofauti na kina cha imani ambayo imetawala katika nyoyo za waifuatao dini hii tukufu. 
Waislamu wametoka  pande zote duniani na kufika sehemu takatifu (Makka).
Huu ni msingi mkubwa usio na mfano unaopaswa kufahamika katika msimu huu wa hija.
Ufahamu huu utasaidia Waislamu kujua nafasi yao ulimweguni, leo na kesho, kisha wajitahidi kufikia nafasi hiyo.
Mwamko wa Uislamu  na kusambaa  katika dunia ya leo ni ishara ya uhakika unaotoa  matumaini   kwa Waislamu.
Uislamu umepata matumaini makubwa  hasa baada ya kupatikana  Mapinduzi ya Kiislamu na kutengamaa kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Umma wetu mtukufu wa Kiislamu ulianza kupiga hatua kwenda mbele na kuondoa uzio uliowekwa na Wagharibi wapitao.
Uzito wa mbinu za madui wa Kimarekani na jitahada zao katika  kutoa   hazina kubwa  dhidi ya  Uislamu.
Kwa kutumia dalili za utandawazi na maendeleo, propaganda ya madui kuhusu Uislamu na ugaidi na jitihada zao katika kuhakikisha kuwatofautisha Waislamu  na kuweka chuki za kimadhehebu.
Kutengeneza uongo na fitina kwa anuani ya ushia kwa ajili ya usuni, pia kwa anuani ya usuni kwa ajili ya ushia, kuanzisha uadui baina ya nchi za Kiislamu na kujitahidi katika kuzidisha khitilafu na kuzibadili khitilafu hizo kuwa ni uadui, pia kueneza  magomvi yasiyo na mwisho na kutumia vyombo vya habari na kijasusi kwa lengo la kueneza ufisadi  na maovu kwa vijana.
Haya yote na mengineyo ni kwa ajili ya kushindana na miundombinu na mifumo makini  iliothibiti katika Uislamu kuelekea utukufu na uhuru.
Hivi sasa ni tofauti na miaka thelathini iliyopita kwa kudhani kuwa Wazayuni  ni nguvu isiyowezekana, tofauti na zama zilizopita kuwa Wamarekani na Wazayuni walikuwa wakijiamulia kuhusu muelekeo wa mashariki ya kati, ni tofauti  na zama zilizopita kwamba; kurutubisha   yuraniyem  na kutengeneza nyuklia na fani zinginezo ngumu katika nchi za Kiislamu, kwani hivi sasa fani hizi ni haki ya kila mwenye uwezo nazo.
Hivi sasa mashujaa wa mapambano ya Palestina na Walebanoni ambao waliwashinda Wazayuni katika vita ya siku 33,  pia Wairani ambao wamekuwa siku zote ni washika bendara ya kupinga uonaevu wa mabavu na ukandamizaji, ni ishara ya kuelekea katika kilele cha ukamilifu.
Kushindwa kwa Wamarekani nchini Afghanistani na Iraq pamoja ya kuwafanyia vibaya wananchi wa Iraq hivi sasa (Wamarekani) wapo katika hali ya kushindwa na kuwaachia wenyewe nchi yao.
Vita dhidi ya Uislamu  katika karne mbili zilizopita mataifa na nchi za Kiislamu, zilikuwa zikidhulumiwa na kuporwa rasilimali zao.
Hivi sasa wanashuhudia kutoka kwa madhalimu hao na kusimama wenyewe kidete kwa ajili ya kuendesha mambo yao wenyewe.
kwa Upande mwengine tunashuhudi harakati za muamko wa Kiislamu unaendelea siku baada ya siku.
Mazingira haya yana matumaini na ishara njema kwa Waislamu.
Hivyo basi inatupasa sisi Waislamu na mataifa ya Kiislamu tuwe wenye kujitahidi kuelekea mustakabali mwema.
Pamoja ya kuwa hotuba hii ni kwa ajili ya watu wote kwa ujumla, lakini matarajio yangu hasa kwa Wanazuoni na Maulamaa wa dini, makundi ya kisiasa na wanafikra wa vioni na vijana ni bora zaidi kuyazingatia haya  kuliko wengine na ndio wanaotakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuyafanyia kazi. 
Quran tukufu inasema: (‘’mmekuwa umma bora (katika watu) mnaamrishana mema na mnakatazana mabaya, na kumuamini Allah Muumba’’)
Umma bora katika aya hii ina maana ya uwanadamu, lengo la kupatikana umma huu ni kuokoa ubinadamu, na jukumu lao ni kuamrishana mema na kukatazana mabaya na hakuna jema bora zaidi kuliko kuokoa umma kutoka katika mikono ya madhalimu, na hakuna baya zaidi kama kuungana na kutumikia  dhulma na ubabe.
 
Wassalam alaykum.
Sayyed Ali Hussen Khamenei
1, Dhul Hijja 1431 (A.H)
8/11/2010 (A.D) 


| شناسه مطلب: 11435







نظرات کاربران