Radiamali ya AFP kwa barua ya Kiongozi Muadhamu Radiamali ya AFP kwa barua ya Kiongozi Muadhamu Radiamali ya AFP kwa barua ya Kiongozi Muadhamu بعثه مقام معظم رهبری در گپ بعثه مقام معظم رهبری در سروش بعثه مقام معظم رهبری در بله
Radiamali ya AFP kwa barua ya Kiongozi Muadhamu Radiamali ya AFP kwa barua ya Kiongozi Muadhamu Radiamali ya AFP kwa barua ya Kiongozi Muadhamu Radiamali ya AFP kwa barua ya Kiongozi Muadhamu Radiamali ya AFP kwa barua ya Kiongozi Muadhamu

Radiamali ya AFP kwa barua ya Kiongozi Muadhamu

Shirika la habari la Ufaransa AFP limetoa ripoti na kusema kuwa, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewaandikia barua ya pili vijana wa nchi za Ulaya na Marekani na kulaani viwango vya kindumilakuwili vya Magharibi. Shirika hilo limeandika: &quot

Shirika la habari la Ufaransa AFP limetoa ripoti na kusema kuwa, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewaandikia barua ya pili vijana wa nchi za Ulaya na Marekani na kulaani viwango vya kindumilakuwili vya Magharibi. Shirika hilo limeandika: "Katika barua hiyo iliyosambazwa kwa lugha za Kiingereza na Kifaransa, Kiongozi wa Iran amesema: Mtu yeyote mwenye mapenzi na ubinadamu huathirika na kuumia anapoona jinai za kigaidi, ni sawa tu jinai hizo ziwe zinatokea Ufaransa, au Palestina, au Iraq, au Lebanon au Syria." Shirika hilo limeendelea kuandika: "Kiongozi wa Iran amelaani siasa zinazogongana za Marekani katika kuanzisha, kulea na kuyapa silaha makundi kama al Qaida, Taliban na makundi mengine ya kigaidi na kusisitiza kuwa, leo hii ugaidi ni machungu yetu sote." Inafaa kukumbusha hapa kwamba, jana, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliwaandikia barua ya pili vijana wa nchi za Magharibi. Barua hiyo imetarjumiwa kwa lugha mbalimbali hai duniani, ikiwemo lugha ya Kiswahili na inapatikana katika mtandao wetu wa Intaneti wa kiswahili.irib.ir. Maelezo zaidi kuhusu barua hiyo mtayasikia baada ya taarifa hii ya habari.

 

 

 

 


| شناسه مطلب: 13384







نظرات کاربران