Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Muqawama ndio njia ya kufidia kubaki nyuma nchi za Kiislamu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Muqawama ndio njia ya kufidia kubaki nyuma nchi za Kiislamu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Muqawama ndio njia ya kufidia kubaki nyuma nchi za Kiislamu بعثه مقام معظم رهبری در گپ بعثه مقام معظم رهبری در سروش بعثه مقام معظم رهبری در بله
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Muqawama ndio njia ya kufidia kubaki nyuma nchi za Kiislamu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Muqawama ndio njia ya kufidia kubaki nyuma nchi za Kiislamu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Muqawama ndio njia ya kufidia kubaki nyuma nchi za Kiislamu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Muqawama ndio njia ya kufidia kubaki nyuma nchi za Kiislamu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Muqawama ndio njia ya kufidia kubaki nyuma nchi za Kiislamu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi: Muqawama ndio njia ya kufidia kubaki nyuma nchi za Kiislamu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema, muqawama ndio njia ya kufidia kubaki nyuma kimaendeleo nchi za Kiislamu na akasisitiza kuwa, eneo lote la Kiislamu ni uwanja wa kusimama kifua mbele muqawama kukabiliana na ukhabithi wa Marekani na washirika wake.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo katika ujumbe kwa Waislamu duniani kwa mnasaba wa masiku ya Hija.


Amesema, kuendelea kuungulika nyoyo zenye shauku ya kuhudhuria ugeni wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu ni mtihani wa kupita tu; na sambamba na kusisitizia ulazima wa kutofifishwa nukta za mafunzo zilizomo kwenye Hija amesema, muqawama wa kukabiliana na madola machokozi na hasa Marekani ni miongoni mwa nukta hizo za mafunzo zilizotukuka.


Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameashiria matatizo na masaibu ya Ulimwengu wa Kiislamu na kueleza kuwa, kujitokeza kifua mbele muqawama na mwamko hususan katika ardhi za Palestina, Yemen na Iraq ni matukio halisi ya eneo yenye kutia matumaini.


Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa: ahadi ya kweli ya Mwenyezi Mungu ni kupata ushindi mujahidina; na athari ya kwanza ya juhudi za jihadi hiyo ni kuizuia Marekani na watumiaji mabavu wengine wasiingilie na kufanya ukhabithi katika nchi za Kiislamu.


Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kuwa: kauli kuu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo imeutia wasiwasi na kuuhamakisha ulimwengu wa Kiistikbari ni mwito wake wa muqawama: muqawama wa kukabiliana na uingiliaji na ukhabithi wa Marekani na madola mengine machokozi; na kushika hatamu za mustakabali wa Ulimwengu wa Kiislamu kwa kutegemea mafundisho ya Kiislamu. Ni wazi kwamba Marekani na washirika wake wanakereketwa na neno "muqawama" na wamehakikisha wanafanya kila aina ya uadui dhidi ya "kambi ya muqawama wa Kiislamu". Kushirikiana nao baadhi ya tawala za eneo ni uhakika mchungu unaofanywa kwa lengo la kuendeleza ukhabithi huo.


Katika sehemu nyingine ya ujumbe wake huo, Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa: kujikakamua kipropaganda Wamarekani kwa lengo la kupotosha ukweli kuhusu azma, takwa na hatua zinazochukuliwa na vijana wenye ghera wa "muqawama" huko Iraq, Syria, Lebanon na nchi nyinginezo na kuwanasibisha na Iran au upande mwingine wowote ni kuwatusi vijana hao mashujaa na wenye mwamko; na hilo linatokana na Wamarekani kutokuwa na ufahamu na uelewa sahihi kuhusu mataifa ya eneo hili.


Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amebainisha kuwa: ni ufahamu huo potofu ndio unaoifanya Marekani idhalilishwe Afghanistan, ambapo baada ya kujiingiza kwake kwa makeke miaka 20 iliyopita na baada ya kutumia silaha, mabomu na makombora kukabiliana na raia na watu wasio na ulinzi, inajikuta imenasa kwenye kinamasi na kulazimika kuwaondoa askari na zana zake za kijeshi. Pamoja na hayo, inapasa taifa la Afghanistan lijihadhari na  nyenzo za kiintelijensia na silaha zisizokuwa za kivita zitakazotumiwa na Marekani nchini humo; na kusimama kidete kukabiliana nazo kwa uwerevu.


Ayatullah Khamenei ameeleza kwamba: wananchi wa mataifa ya eneo wameonyesha kuwa wameamka na wako hadhir na njia na muelekeo wanaofuata ni tofauti kabisa na wa baadhi ya tawala ambazo, ili kuendelea kuiridhisha Marekani, zinatii matakwa yake hata katika suala muhimu zaidi la Palestina.../


| شناسه مطلب: 107573
سواحلیمطالب مرتبط

نظرات کاربران