Message of Imam Khamenei on 2022 Hajj pilgrimage, in SWAHILI
On the occasion of the Hajj season, the Leader of the Islamic Revolution Ayatollah Seyyed Ali Khamenei issued an important message to the all Muslim brothers and sisters attending Hajj rituals. The following is the full text of Imam Khamenei's message to the 2022 Hajj Pilgrimage in Swahili.
Katika ujumbe wake kwa mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, nchi za Magharibi zenye kiburi zimezidi kudhoofika siku baada ya siku katika eneo letu nyeti, na hivi karibuni katika dunia nzima.
Katika ujumbe huo uliosomwa mapema leo kwa mahujaji huko kwenye uwanja wa Arafat mjini Makka, Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa, hii leo uliberali na ukomunisti, zikiwa zawadi muhimu zaidi za ustaarabu wa Magharibi, havina tena mvuto wa miaka mia moja na miaka hamsini iliyopita, sura na hehima ya demokrasia ya Kimagharibi inayotegemea pesa inakabiliwa na maswali mazito, na wanafikra wa Kimgharibi wanakiri kwamba wanateseka kutokana na kupotoshwa kiakili na kiutendaji.
Ayatullah Khamenei amesisitiza kuwa, mfadhaiko na kushindwa kwa Marekani na mshirika wake mtendajinai, yaani utawala ghasibu wa Israel, katika eneo la Magharibi mwa Asia, kunaonekana waziwazi katika medani ya matukio ya Palestina, Lebanon, Syria, Iraq, Yemen na Afghanistan.
Huku akiashiria matunda adhimu za kukua kwa mwamko na kujitambua kwa Kiislamu na vilevile kuibuka muqawama na mapambano, Kiongozi wa Mapinduizi ya Kiislamu amebainisha kuwa, uwanja wa Palestina ni moja ya madhihirisho ya jambo hilo la ajabu ambalo limeweza kuutoa utawala ghasibu wa Kizayuni katika hali ya hujuma na majigambo hadi katika hali ya ulinzi, na kuutwisha matatizo mengi ya kisiasa, kiusalama na kiuchumi. Amesema, mifano mingine angavu ya Muqawama inaweza kuonekana waziwazi huko Lebanon, Iraq, Yemen na baadhi ya maeneo mengine ya dunia.
Ayatullah Khamenei amesema kuwa, hii leo dunia inashuhudia kielelezo chenye mafanikio na mfano wa kujifaharisha wa uwezo na mamlaka ya kisiasa ya Uislamu katika Iran ya Kiislamu. Ameongeza kuwa: Katika kilele cha orodha ya misingi hiyo ya kimsingi, kuna utawala wa Uislamu katika kutunga na utekelezaji wa sheria, kutegemea kura na maoni ya wananchi katika masuala muhimu ya kiutawala ya nchi, uhuru kamili wa kisiasa na kutokuwa tegemezi kwa madola ya kidhalimu. Amesisitiza kuwa, kanuni hizi zinaweza kuwa mahali pa maafikiano baina ya mataifa na serikali za Kiislamu na kuufanya Umma wa Kiislamu kuunganishwa na kushikamana katika mwelekeo na ushirikiano wake.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja umoja na masuala ya kiroho kuwa ni misingi miwili mikuu ya ibada ya Hija na mambo mawili ya heshima na saada kwa Umma wa Kiislamu.
Amesisitiza kuwa, Ulimwengu wa Kiislamu umejaa vijana wenye ari na utanashati, na kwamba mtaji mkubwa zaidi wa kujenga mustakbali ni matumaini na hali ya kujiamini, ambayo hivi sasa inazidi kushamiri katika Ulimwengu wa Kiislamu hususan katika nchi za kanda hii. Amesema: "Sisi sote tuna wajibu wa kulinda na kuzidisha mtaji huu."
Ujumbe kamili wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi huko Arafa mjini Makka utakujieni baada ya taafia hii ya habari.